Saturday, September 13, 2014

WAKULIMA WAPATIWA MAFUNZO YA USINDIKAJI


Shirika la FASO chini ya ufadhiri wa shirika la ILO kupitia The Foundation for Civil Society wametoa mafunzo ya usindikaji kwa wakulima katika kata ya KAHE. Huu ni mwendelezo wa mradi wa kuelimisha wakulima vijana juu ya kilimo cha mbogamboga, na usindikaji. Katika mafunzo hayo wakulima wapatao therasini walipatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kuanza usindikaji lasmi kupitia chama chao cha KAHOCOSO. Mafunzo hayo yaliwezeshwa na Afisa Kilimo Moshi vijijini, (Horticulture) Bi. Mercy Urio na Bi. Modesta Mosha kutoka shirika la SIDO.


Afisa Kilimo Moshi(V) akiwa katika maandalizi ya somo la usindikaji.




Calvin Salema (Mwasibu wa Mradi-FASO) akishiriki katika maandalizi ya somo la usindikaji.


Nyaya zilizolimwa na wakulima hao tayari kwa usindikaji.


Maandalizi ya usindikaji yakiendelea.


Calvin Salema, mhasibu wa FASO akishiriki katika usindikaji


Wakulima wakichemsha nyanya tayari kwa usindikaji.


Mbogamboga zilizoandaliwa kwaajili ya usindikaji




Kifaa cha ukaushaji (solar dryer) kilichotumika katika ukaushaji wa mbogamboga.
M
Mbogamboga zikiandaliwa kwa ajili ya usindikaji.
Mboga mboga zikiweka katika solar dryer tayari kwa ukaushaji.


Mbogamboga zikiwekwa katika Solar dryer.


Nyanya zilizosindikwa zikiwekwa katika chupa tayari kwa matumizi.


Wakulima wakiifadhi nyanya zilizosindikwa tayari kwa matumizi


Madhumuni
Madhumuni ya semina hii ni uwawezesha wanakozi washiriki kuelewa sheria na kanuni za msingi katika kusindika vyakula.
  1.  Kuweza kutambua vifaa vinavyofaa
  2. Kuweka kuelewa usafi na mpangilio wa kiwanda
  3. Kuelezea matatizo yanayoweza kutokea kwa walaji kama usafi na usalama hauzingatiwi katika utengenezaji vyakul
  4. Kuweza kuorodhesha kanuni zausalama na kutengeneza vyakula bora
Mwezeshaji alisisitiza Kazi za kufungasha ni pamoja na kulinda chakula kutokana na:-
  1. ·         Kupoteza au kuchukua unyevu
  2. ·         Kupoteza hewa ya “carbon dioxide”
  3. ·         Kuchukua hewa ya ‘oxygen’
  4. ·         Uchafu, vumbi, udongo n.k
  5. ·         Kusagika, kupondeka n.k
  6. ·         Joto
  7. ·         Chembechembe wasiotakiwa/waharibifu
  8. ·         Wadudu, ndege na panya
  9. ·         Kupoteza au kuchukua harufu
  10. ·         Kuzuia mafuta n.k
Ufungashaji (Packaging)
Mwezeshaji vilevile alisisitiza kuwa katika uuzaji vyakula katika soko, ufungaji una umuhimu mkubwa katika maeneo ya mijini, kwenye ushindani mkubwa wa kuuza bidhaa, ufungashaji mzuri unatakiwa. Vyombo vinavyotumiwa kufungasha lazima view na maombo mazuri na ujazo ambao soko linataka.
Pia lebo ziwe zenye rangi na mpangilio wa kuvutia, pamoja na vielelezo vya kutosha kukidhi sheria za udhibit wa vyakula, Kama vile bei, anwani ya msindikaji, vilivyomo na tarehe za kutengeneza/kutumia bila kuharibika.
Mahita ya kufungasha vizuri yanaweza kuwa kazi kubwa kwa wazalishaji wadogo, maana gharama zake ni kubwa. Hata hivyo, kufungasha kukidhi matakwa ya walaji na sheria ya nchi ni muhimu. Vifungashio viko aina nyingi lakini vinavyotumiwa sana kufungasha vyakula vilivyosindikwa ni kama vifuatavyo:
  1. ·         Chupa na vyombo vya kioo
  2. ·         Chupa na vyombo vya plastic
  3. ·         Vyombo vya aluminium
  4. ·         Makopo na galoni za bati
  5. ·         Mifuko ya karatasi na plastic
  6. ·         Makasha ya karatasi
Miundo mbalimbali ya vyombo hivi inakidhi mahitaji mbalimbali kutegemea sifa za chakula na matakwa ya soko.
Kadhalika mifuko ya ‘plastic’, karatasi, ‘aluminium’ n.k. kutumiwa kufungasha vyakula mbalimbali kama vile vya maji na unga.
Makasha na maboksi ya uwezo mbalimbali yananunuliwa kufungasha bidhaa kwa soko la reja na jumla.